TUWASILIANE KWA E-mail: mobinsons@yahoo.com.

Friday, June 8, 2007

म्ताज़ामो वान्गु किफिक्रा.

Fikra zangu kimtazamo.

Uchaguzi ndani ya ccm na mstakabali wa taifa letu.

Na Mwandishi wetu.

HALI ya uchaguzi wa nafasi mbalimbali ndani ya chama cha Mapinduzi inayoendelea imeonyesha jinsi mwenendo na mstakabari wa Taifa hili unapoelekea, katika uchaguzi huo tumeshuhudia mambo mawili muhimu yakitokea.

kwanza tumeshuhudia watu kutoka sekta na taasisi mbalimbali wakikimbilia barabara ya Lumumba Ofisi Ndogo ya Chama cha Mapinduzi (CCM)Dar es Salaam, kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali, pia tumeshuhudia wajukuu wa vigogo wakigawana fomu jambo ambalo limeibua gumzo.

huku vyombo vya habari vikifanya kazi ya kukitangaza Chama hicho kikongwe kwenye jamii bila kujua kuwa kazi hiyo ilipaswa ifanywe na katibu mwenezi au katibu Mkuu wa chama hicho.

ninasema kuwa vilifanyakazi ya kukitangaza chama hicho kwasababu mara nyingi tumekuwa tukishuhudia vyama vingine vya siasa vikifanya uchaguzi lakini hatuoni habari zao zikiandikwa wala kupewa kipaumbele kama CCM, kwa mfano ni chombo gani kinaandika habari kuhusu uchaguzi unaoendelea katika chama cha CUF?

wakati vyombo vya habari vikifanyakazi ya kukitangaza CCM katibu Mkuu wake Yusuph Makamba aliwaita wanahabari Lumumba na kuwakemea kweli kweli kwa nini miongoni mwao wanaandika mabaya ya CCM, kisha akawaonya wasiungane na wapinzani na kuwafundisha namna ya kuipamba CCM!

Makamba alitumia udhaifu uliopo wa vyombo vya habari kuwaonya wanahabari na kweli baada ya kuondoka wakaenda wakaandika kama alivyoagiza, nasema huo ni udhaifu kwani ilipaswa habari zile wandishi waziache lumumba pale pale na kesho yake angewatafuta nakuwaomba radhi kwa kumsusia.

lakini yangu sio hayo lengo nikutaka kupambanua mambo mawili makuu yalijili katika chama hicho, kwanza imeonekana wazi kuwa Sehemu Mhimu ya jamii imeegea katika chama hicho hiyo ni pamoja na watu mhimu kutoka sekta mbalimbali waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.

Wakati katika Vyama vingine vya siasa imekuwa ni kama dhambi mtu mwenye kazi serikalini au kwenye tasisi kujitokeza wazi tena mchana kuchukua fomu ya kugombea nafasi katika vyama hivyo lakini kwa CCM ni kama sifa au ‘utukufu.’

Wengine tumeshangazwa na habari za utitiri wa wanahabari kukimbilia fomu za kugombea nafasi mhimu ndani ya chama tawala, kimaadili wanahabari Tanzania tumepotoka na kuikatisha jamii yetu matumaini.

Nchi kama ya kwetu ambayo inaoenekana kuwa Democry ni sawa na kupanda mimea katika eneo lisilo na Rutuba kutokana na Vyama vingi kushindwa kuhimili Mikiki mikiki ya CCM, kwa hiyo wanahabari ndio walitegemewa kuchukua nafasi hiyo ya kuikosoa serikali inapotokea wakaomba Ajira CCM jamii itegee nini?

Miongoni mwa wanahabari ambao wamekuishachukua fomu za kuomba kazi CCM ni, Shyrose Banji huyu ni mwanahabari na afisa uhusiani wa Benki ya makabwela NMB, Manyere Jacton huyu ni Mhariri wa gazeti la Mtanzania na baadhi ya wanahabari wengine…

Pia yupo mshauri wa masuala ya sanaa wa kundi la Tanzania One Theatre (TOT) ambaye pia ni mjumbe wa Baraza Kuu Taifa Umoja wa Vijana (UVCCM), Salim Khamis Salim (Chicago) alirudisha fomu za kugombea nafasi ya ujumbe Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi NEC.

Kadhalika naye Malikia wa mipasho nchini ambaye ni mahiri wa kuimba muziki wa mwambao taarab ambaye ni mwimbaji mkongwe wa Tanzania One Theatre (TOT),Khadija Omar Kopa jana alirudisha fomu.

"Natetea nafasi yangu ya ujumbe wa NEC Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), hivyo baasi nawaasa wanawake kuwa tusibaki nyuma hasa wasanii tujitokeze ili siku moja nasi tuwe viongozi na kuendeleza sanaa yetu katika ngazi za juu pia lengo langu la kugombea tena ili nitetee tena ilani ya CCM " anasema Kopa.

Wakongwe wengine wa sanaa waliorudisha fomu zao ni Diwani wa Kata ya Hananasifu Kinondoni Abbas Tarimba huyu ni mwamichezo amewahi kuwa kiongozi wa yanga, Mkurugenzi wa TOT na Mbunge wa Mbiga Magharibi John Komba, Meja mstaafu ambaye ni Katibu Mkuu wa TOC Filbert Bayi.

Wengine ni mtunzi mkongwe wa mashairi na vitabu ambaye alianza kutunga tangu mwaka 1954 Amiri Andanenga ambaye anagombea NEC wazazi.

Hao ni baadhi tu ya watu wanaotegemewa na jamii ambao katu hawawezi kujkitokeza mchana ili kugombea nafasi katika vyama vingine wakiogopa kupoteza nafasi ya kazi zao.

Lakini hata kama ni haki ya kikatiba ya kila mtu kugombea nafasi anayoona inamfaa lakini sio kwa nchi kama ya kwetu hii wanahabari kuingia katika kinyan’ganyiro cha kuomba kazi CCM, hivi mwandishi ambaye ni kada wa CCM anaweza kuandika maovu yaliyo ndani ya CCM.

Kama mwandishi mwanadamizi ni kada maarufu ndani ya CCM itabidi abane chombo chake kisiripoti, vitendo vya rushwa na ufisadi unaofanywa na viongozi wa CCM walio ndani ya serikali akijua kuwa kundika habari hiyo ataitwa na kamati ya maadili kuhojiwa pia wenzake watamtuhumu kuwa anaendekeza siasa za makundi.

Hakuna sababu yoyote ya maana ambayo wanahabari wanaweza kuileleza jamii ikawaelewa kuhusu sababu iliyowasukuma wakagombea nafasi katika chama cha CCM, walitakiwa wakae mbali ili waandike kinachoendelea humo.

Kutokana na hali hiyo tunaona sio vema kuendelea kuitumikia jamii huku wamekalia kiti cha siasa, nivema watumie busara wajiuzulu kwanza kazi ya habari hadi uchaguzi utakapomalizika, kwani jamii haina imani nao tena.

Lapili kataka kinyang’anyiro hicho ni tabia ya watoto wa vigogo ambao tunawaona kama wajukuu wa vigogo kutokana na wengi wao kuwa mababu zao waliwahi kuwa viongozi wan chi hii kuchukua fomu kitendo hiki kimeonekana kuzua gumzo.

Lakini katibu mkuu wa chama hicho Makamba alisema kuwa wamefanya hivyo sio kwa msukumko wa wazazi wao bali wanayo haki ya kikatiba kufanya hivyo, ni kweli lakini hayo majibu ya makamba ni mepesi mno yanahitaji uzito.

Hatuamini kuwa kulikuwa na umhimu wa watoto wa vigogo ambao miongoni mwao wazazi wao wanamadaraka makubwa CCM kuyingia nao katika Siasa,hii inaonekana wazi kuwa ni kujaribu kuunda utawala wa kimatabaka na kurizishana uongozi ambapo tabia hii haina tafauti na utawala wa ‘kifalme’

Wakati mwingine huu mtindo ni mbaya kuliko hata utawala wa kichifu kwani katika utawala wa kichifu ni vigumu kumkuta motto anajiandaa kumrithi baba yake wakati yupo hai,hiyo inaweza kuhesabika kama kulenga kumuua Chifu jambo ambalo linaweza kumletea matatizo huyo motto, lakini katika ‘Demoicracy’ ni fahari mzazi kumuona mwanawe anajiandaa kumrithi.

Hivi inaingia akilini kweli kama motto wa kikwete Ridhiwani atakuwa amechukuwa fomu ya kugombea nafasi ya Halmashauri kuu NEC ,CCM atakuwa tena na mpinzani katika nafasi hiyo?hii si ni sawa na kupita bila kupingwa?

Ingawa hao watoto wa wakubwa wanafanya hivyo kwa kutumia haki na uhuru wao wa kikatiba lakini hatuoni umhimu wa kufanya hivyo wasiwasi wetu ni kwamba tutaenedelea kuwaliwa na matabaka Fulani tu.

Kunawatu ambao wazazi wazazi walikuwa viongozi tangu ukoloni wakaendelea kuwaandaa wanao na kuridhishana mikoba ya uongozi hadi sasa vitukuu wao wapo madarakani, kutokana na mwenendo huu motto wa mkulima toka shamba ameki kuwa mtumwa na mshirikishwaji katika maamzi hana sauti wala nafasi katika serikali.

www.mobinday.blogspot.com 0753 399 579 mobinsons@yahoo.com

No comments: