TUWASILIANE KWA E-mail: mobinsons@yahoo.com.

Monday, July 16, 2007

नि उवेकेज़ाजी ओ उपोराजी?

Mitaji ya wawekezaji haiwezi kuodoa umaskini wa ujinga wetu.

Na Mobini Sarya

DUNIA ipo kwenye mapambano ya kupata maendeleo lakini Afrika ipo vitani kwa ajili ya kupambana na umaskini na ujinga ambao umelikwamisha bara hili lisiendele katika nyanja na maendeleo na tekinolojia ingawa limejaliwa malighafi na kila kitu.

Wakati Dunia ikiwa katika vita ya maendeleo Tanzania inaoneka kushindwa kabisa hata ile hatua ya kupambana na ujinga na umaskini , Mapambano ya ambayo yalitangazwa na Rais wa kwanza Mwalimu Nyerere saa chache baada ya kujipatia uhuru kutoka kwa Wakoloni Mwaka 1961.

Askari waliopaswa kupambana katika vita hiyo wamekuwa wakipungua nguvu kila kukicha, wakistaafu na wengine wakifa kama hayati Mwalimu Nyerere alikuwa kamanda wa vita hiyo huku askari wakiendelea wakiendelea kutumia silaha zile zile za mwaka 61.

Siku chache zilizopita niliandamana na viongozi wanne wa vyama vya siasa, TLP,CUF ,CHADEMA na NCCR-Mageuzi katika ziara yao ya Mikoa miwili Kigoma na Kagera wakiwapa wananchi Elimu ya Uraia nikiwa Kagera wilayani Ngara katika mkutano wa Hadhara wananchi walisoma risala ya kushangaza.

Katika mkutano huo uliofanyikia viwanja vya Posta na kuhudhuria na watu mbalimbali katika Risala hiyo iliyosomwa mbele ya Mwenyekiti wa CHEDEMA, Freeman Mbowe ,NCCR-Mageuzi James Mbatia ,CUF Prof Ibrahim Lipumba na Chama cha TLP Agoustne Lyatonga Mrema,

wananchi walisema kuna mgodi eneo la kabanga ambao shughuli zake zimekuwa zikendeshwa kinyemela kwa muda mrefu huku shughuli hizo zikifanywa kwa usiri mkubwa huku wakiwa na taarifa kuwa madini mbalimbali yakiwemo Dhahabu yanachimbwa eneo hilo.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi alishangaza zaidi aliposema kuwa anaifahamu huo mgodi wa kabanga kwani umeanza kudaiwa kufanyiwa utafiti tangu anasoma shule ya msingi miaka 34 baadaye wakati huo wawekezaji walikuwa wanatafiti madini ya Nikel lakini baadaye ulipatikana utitili mwingine wa madini.

Mbatia anasema wakati huo ndege zilikuwa zinatua kila jumatatu na ijumaa kuchukua kile kile wanachoita sambuli ya madini na kupeleka ulaya kwa ajili ya kupima wakati wanasema hayo hakuna kiongozi yeyote wa Serikali katika eneo hilo aliyejitokeza kupina hayo madai lakini yalipofika kwenye gazeti serikali imeyaona kuwa sumu.

Serikali kupitia wizara ya nishati na Madini imetumia kodi za wananchi, kuja juu na kumshutumu mwandishi na gazeti zima kupitia kwenye matangazo yake eti kwanini habari ile iliandikwa bila kuwauliza wao utafikiri mwandishi kaibua.

Katika taarifa yake wizara ya Nishati ilidai kuwa habari iliyoandikwa katika gazeti bila kupata taarifa za kitaalam ililenga kuchochea wananchi kupinga uwekezaji huo wa miaka 34 bila tija, nakuwashauri wahariri na wandishi kufanya itafiti wa kina ‘kama wa mwekezaji kwa muda mrefu’kabla ya kuandika makala au habari kwa umma.

Nakumaliza hasira kwa kusema habari au makala zilizoandikwa bila takwimu au taarifa sahihi zinapotosha baadala ya kuelimisha ufafanuzi huo unaoonekana kuwa shutuma ulitolewa na Kamishna wa Madini Dalaly Kafumu.

Ukisoma ufafanuzi uliotolewa na Kamishna kisha ukalinganisha na madai ya wananchi walioyatoa katika gazeti la Tanzania Daima Julai 9 mwaka huu utabaini kuwa mgodi wa kabanga ambao wizara inasema sio mgodi bali ni eneo la utafiti, kuna jambo ambalo wakubwa wanalificha.

Wananchi walisema kuwa eneo linapatikana madini aina ya Platinum, Nikel ,Uranium,Dhahabu n.k na limefanyiwa shughuli kwa miaka 34 kiinyemela kwa makampuni kadhaa yanayodai kuwa yanadai kuwa yanafanya utafiti huku yakuuziana mikataba kienyeji.

Madai hayo yanadhibitishwa na wizara inaposema kuwa historia ya utafutaji madini katika eneo hilo ilianza Mwaka 1974 wakati ukifanywa na wizara ya maji, nishati na madini chini ya mradi wa utafutaji madini ‘Project no.URT-73/030 uliokuwa unafadhiliwa na shirika la maendeleo UNDP uchunguzi huo uligundua maeneo 48 yanayoonyesha kuwepo madini aina ya Nickel,shaba, Cobalt,chrome na Zink.

Katika eneo hilo wataalam walikadiliwa kuwepo na Nickel tani milioni 26 zenye asilimia 0.7 za nickel, baada ya ugunduzi huo wizara ya nishati inasema makampuni mbalimbali yamekwisha fanya utafiti eneo hilo ambayo ni

Romenex/Sutton Resources, Sutton Resources/BHP ,Anglo America/Sutton Resources na Barrick Gold Corporation /Falconbridge na sasa yaliyopo ni Barrick Gold Corporation kwa Kushirikiana na Xstrata Nickel.

Hapo baada ya wizara kudhibitisha madai alichokikosea mwandishi nini kutoa taarifa kutoka sehemu moja kwenda nyingine au kuiamsha Serikali ilazimike kutoa ifafanuzi kwa Umma kwa sababu tangu madini hayo ,mbalimbali yapatikane serikali haikuwahi kutoa taarifa zozote kwa umma na isingetoa kama habari hizomsingeandikwa.

Lakini wananchi bado wanamashaka ni madini gani hayo ambayo kwa miaka 34 yanafanyiwa utafiti na bado udongo wake unakwenda kupimiwa ulaya bila kinu chake kuanzishwa hapa nchini, kwa maneno yake yenyewe wizara ya madini imezibitisha kuwa kuanzia mwaka 2003 pekee hadi sasa wamesafisha nje tani 13.2 za miamba inayokisiwa kuwa na madini sawa na wastani wa tani 2.6 kwa mwaka!

Katika maelezo hayo ya kushangaza serikali inasema kuwa ili uchimbaji wa Nickel uwe na faida kibiashara unahitaji kuchimba tani milioni 1 za miamba kwa mwaka kwa hiyo kuchukua miamba kiasi cha wastani wa tani 2.6 kwa mwaka hauwezi kuzalisha nikel kibiashara.

Wizara inashindwa kuambia umma kama sio kibiashara hizo tani 2.6 kwa mwaka anakula nani wakishauza uko nje kwani anatuambia kuwa kabla ya kusafirisha nje hizo tani hupeleka kwenye ofisi za madini kanda ya ziwa kukaguliwa na kupewa kibali cha kusafisha nje ya nchi (export Permit) ,lakini hatuambiwi baadaye kama helejeshwa hiyo tani hapa nchini.

Tunadhani majibu yaliyotolewa na wizara yalikuwa mepesi yanayiolenga kuwafurahisha baadhi ya watu hasa katika kipindi hiki cha bajeti, kwani baadala ya kuwafafanulia wananchi waelewe kinachofanyika hapo unaelekeza shutuma kwa mtu asiyehusika,

ni vema taarifa za migodi mingine zikatolewa kwani huo sio wakwanza kuna mwinge huko geita tulisikia kampuni ilifanya utafiti kwa miaka 23 hadi mkuu mmoja alipoingilia katu weka wazi kama wa North Mara makampuni kubadilisha mikataba kinyemela na faida iliyopatikana katiaka mgodi wa Buhemba Mara.

www.mobinday.blogspot.com 0753399579

No comments: