TUWASILIANE KWA E-mail: mobinsons@yahoo.com.

Monday, March 17, 2008

Hii sasa Hatari!! WASABATO WAGAWANYIKA

HIZI NI DALILI TOSHA ZA MWISHO WA DUNIA

Na MCHUNGUZI WETU

HIVI karibuni limeibuka kundi la wasabato wenye msimamo mkali na ya kanisa la wasabato ambao wamekuwa wakihubili ujio wa Yesu Mwezi ujao, na mwandishi wetu Mobini Sarya analichambua chimbuko la kundi hilo.KANISA la Wadventista Wasabato (SDA) ni miongoni mwa Madhehebu yanayojulikana kuwa na msimamo mkali tangu lianzishwe miaka zaidi ya 150 iliyopita baada ya kumeguka kutoka Dhehebu likingine la Babtist kutokana na tafauti za kiimani na kimsimamo.

Kanisa hili kwa sasa limekumbwa na Mgogoro wa kiimani baada ya kuibuka tena makundi mawili yanayotofautiana kimsimamo na kiimani moja likiwa na msimamo mkali zaidi unaotokna na mapokeo ya kale yasiyotaka mabadiliko na lingine likiwa na ule wenye msimamo wa wastani unaotaka mabadiliko.

Kutokana na tafauti hizo zilizojitokeza zimesababisha Kanisa hilo ambalo ni miongoni mwa Makanisa makubwa makongwe hapa duniani na lililokuwa likiheshimika hasa kutokana na msimamo wake huo mkali kugawanyika vipande.

Kundi hilo lenye msimamo Mkali lilianzishwa na Mchungaji Nyagoryo ambaye kwa sasa ni Marehemu na mazingira ya kifo chake yanadaiwa kuwa ya utata.

Katika uchunguzi uliofanywa kwa muda mrefu sasa imeoneka dhahiri na wazi kuwa tofauti iliyojitokeza ni kubwa kiasi kwamba ni vigumu kuweza kupatana na kurudiana kama ilivyokuwa awali hiyo ni kutokana na msimamo wa makundi yote mawili uliyokwisha jengeka baina yao.

Wafuasi wa Mchungaji Nyagoryo wanasema kuwa wameamua kujitenga baada ya kuona mafundisho mageni waliokuwa wakiyapinga ambayo wanayaita ya Rumi (Roma) yameingia kwenye kanisa hilo.

Baada ya kujitenga na kuanzisha kanisa lao pamekuwapo na mkanganyiko wa majina kwani kila Dhehebu linajipa uhalali wa kujiita SDA yaani Seventh-Day Advents Church.

Hata hivyo kanisa linalotambulika sasa hadi serikalini lile linalojulikana kama Seventh-Day-Adventist Association of Tanzania (S.D.A.A.T.)hiyo ni kwa mjibu wa cheti cha usajili wa kanisa hilo kilichotolewa na wizara ya mambo ya ndani February 23 Mwaka 1999 uchunguzi umebaini.

Hilo jina la S.D.A.A.T. linatajwa kuwa ndio limechangia kuvuruga mashikamano wa kanisa hilo, baadhi ya waumini wakihoji kwanini jina hilo libadilike kutoka SDA na kuwa Asociation of Tanzania.

Kwa hiyo waumini waliokuwa wanahoji hivyo wakaonekana wanamsimamo mkali wasiotaka mabadiliko yanayoendana na Dunia ya sasa hivyo wakaamua kujiengua kutoka kanisa hilo kubwa na lenye kuheshimika hapa nchini kutokana na misimamo yake mikali ya kutunza sabato.

Sasa wanajiita kuwa wao ndio wasabato asilia na kundi lao linadai kuchukua jina la Seventh-Day-Adventist Church yaani SDA Church, lakini kwa wasabato hili sio kundi la kwanza kujiengua kuna baadhi ya viongozi wa kanisa hilo wamewahi kutoka na kuanzisha makanisa yao.

Tatizo ya hili kundi lenyewe limeng’ania jina la SDA nakutishia kuwagawa waumini wa kanisa la wasabato ambao wanafuata jina kanisa.

Chanzo cha mparaganyiko huo ulioleta mpasuko hu ni baada ya mafundisho mageni kuletwa katika kanisa hilo ambayo wengine wanayaona kama ya uongo.

Wazee watatu wakundi hilo linaloitwa la msimamo mkali wenyewe wakijiita wasabato wa Marejeo waliozungumza kwaniaba ya mchungaji wao Mtabi, walisema kuwa wameamua kujitenga na kanisa hilo baada ya kuona mafundisho ya uongo yameletwa kanisani humo.

Wazee hao waliyataja mafundisho makuu matano ambayo hayakuwemo awali kanisani humo na sasa yameletwa na yanafundishwa na kulifanya kanisa hilo ligawanyike katika makundi mawili ambayo walisema kuwa kamwe hayataweza kurudiana hadi yesu aje .

Kwanza wanasena kuwa ni kubadilika kwa jina la Kanisa hilo kutoka SDA Church hadi kuwa Association of Tanzania na kujenga hoja kuwa kanisa hilo limejengwa juu ya mitume na manabii Waefeso 2.20 kwa hiyo hakuna mwenye uwezo wa kubadili jina la SDA.

Wanataja kitabu cha selected massage Book UK.383 kitabu hicho kinataja jina hilo kuwa linaonyesha ukweli ambao ni jaribio kwa makanisa mengine kwamba ndio linalotunza sabato yaani SEVENTH-DAY ADVENTST CHURCH sasa imebadilishwa nakuitwa Seventhday Asociation of Tanzania, jina hilo limebadishwa mwaka 99.

“Hapa tafauti ni Church na Asociation of Tanzania na ndio ugomvi wetu mkubwa kwanini wabadili jina tulipohoji wakatuambia ni kwa maslahi ya kanisa kupata misaada toka nje ndio maana wakaamua kubadili jina na kutumia Association jambo ambalo hatulikubali”anasema mzee Chiganga wa kanisa la asili.

Lakini wanakataa kuwa kanisa lao la sasa sio jipya ni lilie la zamani na kutaja baadhi ya vitabu ambavyo vinakataza kubadili jina la kanisa hilo “tunakataa jina jipya la Assocition kwa sababu halipo kwenye maandiko ya Roho ya unabii wala kwenye Biblia”

“Kanisa sasa limeleta mafundisho mapya ambayo kwenye Bibilia hayamo wala kwenye vitabu vya Roho ya unabii”wanasema wazee hao watu huku wakimtajia mwandishi vitabu kadhaa.

Hata hivyo jina hilo linang’ang’aniwa na Makanisa yote mawili kila moja likidai kuwa na uhalali wa kulitumia jina la SDA, hayo yamedhibitishwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na Mchaungaji mmoja wa nisa hilo anayeongoza Mtaa wa Yombo wenye Makanisa nane alipokuwa akiwaelezea waumini wa Kanisa la Karakata, chanzo cha Mgogoro huo.

Madai ya kundi hilo kulalamikia jina yanapingwa vikali na upande wa pili, Mchungaji wa kanisa la Yombo Dar es Salaam, Daniel Mshora alisema wao bado wanaendelea kulitambua jina hilo la SDA,

na kwamba Association linalolamikiwa na waumini ni jina la usajiri tu ambalo kila mtu anayekwenda kusajiri kampuni au tasisi yake lazima asajiri jina la kampuni na la Biashara.

“hatujabadili kanisa kuwa chama kama wanavyodai hao wanalioasi ,bado tunatumia SDA , hilo jina la Association ni la usajili tu wa shughuli zetu kulingana na utaratibu wan chi unavyotaka”alisema Mshona.

Mafundisho mengine wanayoona yameingizwa kwenye kanisa hilo ni kubadilika kwa Nembo ya kanisa hilo kwani nembo ya awali ilikuwa ni Malaika watatu wenye matarumbeta wakipita juu ya ulimwengu wakitoa ujumbe wa onyo ,Nembo hiyo imeandikwa kwenye kitabu cha Salected Massege 2Book uk.385.

kwamba ilitakiwa isibadishwe hadi historia ya dunia ifungwe lakini sasa imeleta Nembo mpya ni Msalaba,Mwenge, kitabu na Jua, wanasema nembo hiyo ilitakiwa isibadilike wala kuondolewa hadi mlango wa rehema ufungwe.

Akitetea Nembo hiyo Mchungaji Mshora alisema kuwa wameamua kutumia Msalaba ambao awali walikuwa wakiupinga baada ya kubaini kuwa ndio ukombozi wao kwani hata mbinguni upo.

“Misingi yetu ni Biblia hadi leo wasabato hatujadaharau ujumbe wa Malaika wa Tatu ila tulichonacho kwa sasa ni Roho kinachowakilisha tasisi ,mashirika na makanisa ambayo kila anayekwenda kusajiri lazima awe nacho”alisema akinukuu Biblia Zaburi 116;105 na Yohana 17;17.


Wasabato hao wa marejeo wanadai kuwa fundisho lingine ambalo lieingizwa kanisani ni Kukatia maisha Bima jambo ambalo wanasema maandiko yanawazuia wasabato wasijihushe na Bima kwani yesu aliposulubiwa msalabani aliwalipia,na kutaja vitabu kadhaa vinavyozuia kujihusisha na swala hilo,Test mon for the church Volume 1 Uk.550 na matukio ya siku za mwisho Uk.144

Hata hivyo suala la Bima linatetewa na viongozi wa kanisa la wasabato kuwa wameliweka ili inapotokea mmunini akapata ajali wakati akiwa kwenye shughuli za Dini aweze kulipwa na shughuli zingine.

wanataja fundisho la nne kuwa ni haki sawa kwa akina mama kanisani na kuliona kama fundisho lingine batili “wameanzisha idara ya wanawake kanisani ambayo inadai haki sawa za kiutendaji ” wanasema wazee hao

nakuzitaja haki hizo kuwa sasa wanawake wakisabato wanapewa uchungaji na uzee wa kanisa jambo ambalo linakwenda kinyume na maagizo ya Mungu

“Mungu amesema usiruhusu mwanamke kufanya kazi za Ofisini wa kupiga kura ,uchungaji ni kazi ya ofisini na hutiwa mafuta 1Wakorintho 14: 34,35 na kuongeza kuwa imeandikwa mwanamke na anyamaze kanisani na watakao ungamikono kazi hiyo ya akina mama watapewa roho nyingine”.wanakariri maandiko.

Jambo lingine wanataja mafundisho yasiyo ya Imani yao kama sababu nyingine ya kuligawanya kanisa hilo ,Msalaba ndani ya kanisa na kuonyesha picha za ukatili wa kirumi zilizochorwa kwenye vitabu vyao na kunukuu kitabu kiitwacho Counsels to Writers & Editors uk.260 na kingine ni Dogma yaani mafundisho yasiyokuwa na swali yachuliwe kama yalivyo.

Pia wanataja kuwa mafundisho ya Liturujia kama mafundisho mengine mapya yaani mafundisho ya kukariri sala na kutoa mfano kuwa hivi karibuni wanawake wa kisabato walipokuwa kwenye Idara yao ya wanawake walikaririshwa sala kwa kutumia vifundo vya mikono.

Wazee hao walisema kwa kukariri kitabu cha pambano kuu Uk 27,28 kuwa Baada ya mapambano ya muda murefu ni lazima kuwepo na utengano hatuwezi kuvumilia kuona makosa hayo mabaya yenye kuleta hatari kwa watoto wao na wajukuu yakindelea Ezek.12;1-
Nakusema kuwa sababu hizo ndio zimefanya waamue kutoka kwenye kanisa hilo kwa uaminifu na hawawezi kudai makasa kwani muda ulio salia dunia ni mchache.

Kwa upande wake kanisa la Association of Tanzania viongozi wake hawakuwa kuzumgumzia mpasuko huo hata alipofuatwa Mwenyekiti wa kanisa hilo mkoa wa mara James Machage alipiga chenga kuwa hana nafasi mwandishi aende siku nyingine alipofutwa tena hakuwa tayari kuongea kwa madai kuwa alikuwa na shughuli za kanisa.
Havi karibuni nusura kwamara ya kwanza katika historia ya kanisa hilo makundi hayo yafikishane mahakamani mjini musoma ,baada ya kundi la wasabato linaloongozwa na Machage kwenda Polisi kustisha kibali cha kundi linaloongozwa na mtabi ambalo kwa sasa mkubwa wake Tanzania ni Mchungaji Nyagori ,kilichokuwa kinawaruhusu kufanya mahubiri ya wiki mbili mjini hapa ilibidi yavunjwe.