TUWASILIANE KWA E-mail: mobinsons@yahoo.com.

Wednesday, March 16, 2011

majina ya waliochaguliwa kidato cha tano yatangazwa

wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi leo imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi vya serikali.

majina hayo yametangazwa na waziri wa elimu Dk.Shukuru kawambwa kufuatia kukamilika kwa uchaguzi uliofanyika mara baada ya kutangazwa ,matokeo ya mtihani wa kidato cha nne.
Dk.Kawambwa ametaja idadi ya wanafunzi hao wanaojiunga na kidato cha tano mwaka huu kuwa ni 36366, wasichana wakiwa ni 11210 na wavulana wakiwa ni 25156.

kwa upande wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya ufundi ni 916 wakiwemo wasichana 861.

aidha Dk.Kawambwa amesema kuwa vigezo vilivyotumika kuwachagua wanafunzi hao ni pamoja na umri usiozidi miaka 25 awe amefaulu alama 3 na ufaulu wa daraja la kwanza hadi 3.
pia wanafunzi waliochaguliwa kwenye fani ya ufundi wanatakiwa wawe wamefaulu masomo yaPCM kutokana na sifa hizo wanafunzi 29 wamekosa nafasi kwa kufuka umri huo.

Waziri kawambwa amesema kuwa wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti April 3 Mwaka huu katika shule walizopangiwa kabla majina ya awamu ya pili hayajataangazwa.

No comments: