TUWASILIANE KWA E-mail: mobinsons@yahoo.com.

Monday, April 30, 2012

WASIOTOKA muungano waanze kuondoka Bara

NI miaka 48 tangu mataifa mawili yaungane na kuanzisha taifa moja lenye nchi mbili, Taganyika na Zanzibar. Tangu waasisi wa mataifa haya mawili Mwalimu Julius K.Nyerere (Tanganyika) na Abeid Aman Karume (Zanzibar) waunganishe mataifa hayo kwa hiari yao na kuunda nchi ya Tanzania April 26 Mwaka 1964, wanaanchi wake waliishi kwa amani na upendo. Hata hivyo zaidi ya Miaka 10 baada ya waasisi hao kutoweka duniani kimeibuka kizazi cha ‘wabengazi’ kinachopinga muungano huo. Wengi wao ni vijana watukutuku wasio na kazi ambao wamekuwa wakishinda katika vijiwe vya wauza kahawa mjini Unguja maeneo ya Mji Mkongwe, Darajani, fukwe za Fuoni na hata kibandamaiti wakipewa uchochezi na vibaraka wa kisharaz ‘wabenghaz’. Eti wanadai nchi ya Zanzibar, lakini kwa mjibu wa tafsiri ya jiografia, nchi ni kanda au eneo la kijiografia.Neno hili mara nyingi hutumiwa kwa kitengo cha kisiasa au eneo la taifa huru, kama ilivyo sasa Zanzibar, hivyo hakuna haja kupiga kelele za kutoa madai yasiyo na sababu za msingi. Kwani sio kila wakati, nchi inapaswa kuwa na eneo huru na kuhusishwa na taifa au Serikali hata kisiwa kinaweza kuitwa nchi kulingana na ardhi yake isiyo na maji. Sasa wanapoibuka watu wanadai nchi ya Zanzibar, tunajiuliza ni nchi gani wanaodai au ni nani amewakalia?, au wanataka taifa huru?. Kwani taifa maana yake ni nini,ni kundi la binadamu lenye utamaduni wake maalumu na mapokeo yake katika historia ya eneo fulani linaunda taifa. Kila mojawapo lina haki kwa kujitambua hivyo na kuhamasisha mshikamano kati ya watu wanaoliunda hata kujipatia uhuru wa kisiasa walau kwa kiasi fulani. Kama tafsiri ya taifa ndio hiyo, kwa nini leo vijana wanaoonekana kama wahuni wanaendelea kutusumbua kwa maandamo ya kupinga muungano, sasa wanataka nini ikiwa Zanzibar inajulikana kama ni nchi na taifa huru ndani ya muungano. Je, kama hawa wanaopinga muungano wakifanikiwa adhama yao,wanawezaje kutuhakikishia kuwa hawana nia ovu ya kuitoa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuipeleka utumwani kwa Sultani wa Umoja wa Falme za Kiarabu kupitia OIC?. Wakazi wengi wa Zanzibar waliozoea matunda ya muungano, wameanza kubadilika tabia zao baada ya kupewa maneno ya kichochezi yanayofanywa na makundi ya vibaraka kwa jina la wanauamsho. Wanajificha katika kivuli cha uhuru, demokrasia na uzalendo. Wanajiita uamsho kwani wameambiwa ‘Wazanzibari’ wamelala, sasa wanataka kuamshwa au ni uchochezi kama ule uliofanywa katika mji wa Benghazi nchini Libya, baada ya vijana wengi kupewa madawa ya kulevya na bangi kutoka kwa mawakala wa CIA ili wamng’oe kiongozi wao mpendwa, Hayati Mohammad Gadhaffi. Lakini kinachoshangaza katika kupinga muungano, wao wanakataza hadi wabara kuhamia kule au kufanya kazi Zanzibar tena wanataka kupenyeza ajenda za kisheria kuwanyima ajira wabara,bila kutambua kuwa wao ni kisiwa kidogo ambacho kinalingana na kisiwa kingine cha Ukerewe kilichopo katika ziwa Victoria. Lakini pia kwa upuuzi wao (wapinga muungano), wanapaswa watambue kuwa kama wanaupinga muungano nao wawe tayari kuhama bara, Watanganyika watakapoamua kujibu?. Nimeandika kuwa, wanaopinga muungano ni vikundi vya wavuta bangi vinavyoongozwa na watuhumiwa wa uhaini Zanzibar, wengine wamewahi kuswekwa ndani kwa tuhuma za kumuua mmoja wa waasisi wa muungano huo, ndio hawajiulizi kwanini Wazanzibari wengi wanahamia sana bara. Muungano hata leo ukivunjika Watanganyika hawana cha kupoteza zaidi yao, wamehamia bara, wananunua ardhi kubwa, wanalima, wanafanya biashara sana za kila aina, halafu leo wanaibuka nakudai kuwa hawataki muungano, ondokeni haraka tuone jinsi mtakavyohamisha majengo yenu kariakoo na mashamba ya Kongowe!. Siamini kama wanaopinga muungano wanaakili timamu, kwa sababu ukifika Dar es Salaam, utawakuta wapemba ndio ‘whole sale’, ‘retain’, daladala, taxi, kilimo hata ndani kabisa vijijini Morogoro hadi Ulanga, Bagamoyo, Mkoa wa Tanga na vitongoji vyake. Iweje leo wajitape kuwa hawataki muungano wakati hata bandari bubu za kuleta biashara zao kutoka Zanzibar zimejaa Bagamoyo, Pangani, Mkuranga, Rufiji na Kilwa. Serikali inakosa kodi kwa bandari zao bubu hizi ambazo pia huenda hupitisha madawa ya kulevya, lakini tunasema kwamba ni wenzetu na hayo ndio matunda ya muungano, kubembelezana kunaelekea kufika mwisho. Ni nani mzigo kwa mwenzake kati yetu?.Wazanzibari wamekuwa wakishiriki katika biashara ovu ya ukataji wa mikoko, mbao na fito zake husafirishwa kwenda Uarabuni, tunawaacha sasa wanatudharau na kuona wenzao hawafai. Ni nani aliyewaloga nyinyi wapinga muungano?. Nani anabisha kuwa maeneo mengi Pwani mfanyabiashara mkuu sio Mzanzibari na zaidi ni Wapemba?.Ndio wenye biashara kubwa, majahazi na mashua kubwa. Mafia imevamiwa vibaya na uvuvi haramu, waendeshao shughuli hiyo huku bara wengi ni Wazanzibari hata ndani ya maegesho ‘Marine Park’.Katika maeneo mengi ya Zanzibar mazingira yanatunzwa, lakini ukataji mikoko ni huku Bara kwa ajili ya kukarabati majahazi. Mvuvi akija bara, akijipatia mke anaweka Kambi Tanganyika, kwa sababu hatotakiwa kule na wake wenzie sababu ya ubaguzi wao unaoendelea kuwatafuna. Kuna mambo mengi ambayo wabara wako kimya hawayaongei wazi, wanasubiri Wanzanzibari wachochee mjadala halafu wabara wawambie kama wanajitenga jitengeni haraka, basi ili wakija bara waje kama wawekezaji, tuanze kukusanya kodi za majengo na mashamba yenu Pwani. Kuna msemo usemao 'Kwa somo kunaliwa na kwa mwali pia kuliwe!.Kama ni suala la visima vya mafuta-mbona huku bara vipo vilivyogunduliwa na kuweka alama tangu Mwaka 1952-54?. Mwasisi wa taifa hili Baba wa taifa, alisema hatochimba madini, mfuta mpaka vijana wake wasome ili waifanye kazi hiyo kwa utaalamu. Tungekuwa tumeanza kuchimba mafuta baada ya taifa hili kupata wasomi wengi, lakini tatizo ni kwamba wenye hela wanafadhili vyama vya siasa na mipira sio ununuzi wa mashine za kuchimba mafuta na kusaidia wasomi wenye kupenda kazi. Ili waunde kampuni ya uchimbani mafuta, madini na hao matajiri kugharimia wataalamu kutoka nchi za nje ili kampuni ya wahandisi wetu na wana madini wasomi wa Tanzania wajichimbie mafuta kulifanya taifa liwe na uchumi endelevu. Watanganyika watajirekebisha lini?.Sichochei kwamba Watanganyika wajirekebishe kwa namna ya kujibu mapigo nao wadai kama wenzao wanavyodai ama wawafukuze ndugu zetu, bali uonevu unaofanywa na ndugu zetu watupande kichwani, mtusi na kejeli vinaweza kufika kikomo.Tuchukua tahadhari tusifike huko. Wanadai wanaonewa wao wanataka kujitenga! Wanaonewa kivipi?.Tumekuwa ‘bize’ kuuza chips, vitumbua barazani, vioski vya pombe na kuwaacha wajao toka visiwani kuchukua ardhi na kufanya kweli. Lakini "Mtoto akililia wembe-Mpe, acha waanzae wao kuandamana,wenzao nao kuandamana kuwapa saa 24 wawe wamehama, hapatakalika.Kila jambo linazama zake za utiifu ujinga,upole,uvumilivu,uungwana na wendawazimu. ‘Eh Mwenyezi,Mungu wa Tanganyika’, Mwenye hekima aturehemu, atuongezee upendo na busara tuwe wavumilivu, tuishi nao ndugu zetu, awape pia kumbukumbu ya historia ya nchi ya Utumwa na kuwa aliyepo kule kisiwani alitolewa nchi mbali mbali hata huku bara na ni ndugu zetu wa damu. Vingenevyo wenzao watakapoamua kujibu wasiwalaumu, kwani wataanza kwa kuwapa muda wahame wote bara kisha watahamisha wanajeshi wao walioko huko, tamaa itawashika vijana watataka kushika dola kwa ghasia, CIA itasema Zanzibar sasa ni kisiwa cha magaidi hapo tutaanza kushuhudia tani za mabomu zikidondoka kama ilivyo Somalia, Sudani na Eritrea, thubutu!. www.mobinday.blogspo.com 0656 938316

No comments: