TUWASILIANE KWA E-mail: mobinsons@yahoo.com.

Sunday, May 11, 2014

Mafua ya kuku yalipuka yashambulia bagamoyo


Na Mobini Sarya,Tanpress

Ugonjwa wa mafua ya ndege umelipuka na kuathiri ndege wakiwemo kuku katika jimbo la Chalinze mkoani Pwani.
Afisa Kilimo na mifugo Kijiji cha Saleni Kata ya Lugoba wilayani, Bagamoyo,Rashid Ali Ramadhan,amesema kuwa tayari kuku kadhaa wamekwisha kufa huku ugonjwa huo ukizidi kusambaa haraka.


“Huu ni ugonjwa ambao unatusumbua katika ukanda huu wa pwani kila mara hivi sasa umelipuka na wafugaji wengi wamepata hasara”anasema Ramadhani
Akiuelezea ugonjwa huo anasema kuwa wakulima wanaofuga kuku wanapaswa kuwachanja wakiwa na wiki nne tangu wazaliwe ili kuweza kudhibiti maambukizi.
Ramadhani anasema kuwa kuku au ndege akishapata ugonjwa huo macho huvimba na kupofuka hivyo kushindwa kula chakula na baadaye hufa kwa njaa.
Baada ya kuku kuugua mfagaji anatakiwa kumsafisha kuku macho kwa kutumia mafuta ya kula na kumpaka mafuta ya taa kila mara ili awe kuona chakula vingenevyo anakufa na njaa.
“hakuna dawa nyingine ambayo anaweza kupewa lakini kama bado ni mdogo unaweza kumchanja dawa  aina ya Chicken pox Vaccine,..uhakika ni asilimia 80 kwamba hawataugua ugonjwa huo”anasema Rashid
Aidha mmoja wa wafugaji wa kuku ,Seleman Hamad ambaye ana kuku zaidi ya 600, amesema kuwa awali wataalum wamuilwambia kuwa ugonjwa huo ni ndui lakini baada ya kwenda nao kwa wataalam wengine akabaini kuwa ni mafua.
“Waliponiambia kuwa ni ndui nikajiuliza mbona nilikwisha chanja , lakini baada ya kuwapiga picha na kwenda nao katika maduka makubwa ya karaiakoo, wataalm walipoona tu wakaniambia ni mafua ya ndege na kweli nilipoanzisha tiba wameanza kupona”anasema Hamad.

No comments: