TUWASILIANE KWA E-mail: mobinsons@yahoo.com.

Sunday, May 11, 2014

Ufugaji wa kuku ni utajiri wa haraka,magonjwa ni kikwazo
Na Mobini Sarya,Tanpress

WAKATI kuku wakiendelea  kuteketea kwa kuvimba macho,kupofuka na kutoa makamasi hatimaye kufa watalam wa mifugo wamepishana kauli kuhusiana na aina ya ugonjwa huo.
 katika maeneo ya vijiji  mbalimbali  vya jimbo la Chalinze,mkoani Pwani wataalum,wafugaji wa kuku wamepata hasara baada ya kuku wao kupoteza maisha baada ya kupofuka na kushindwa kuona chakula.
Afisa Kilimo na mifugo Kijiji cha Saleni Kata ya Lugoba wilayani, Bagamoyo,Rashid Ali Ramadhan,amesema kuwa tayari kuku kadhaa wamekwisha kufa huku ugonjwa huo ukizidi kusambaa haraka.

“Huu ni ugonjwa ambao unatusumbua katika ukanda huu wa pwani kila mara hivi sasa umelipuka na wafugaji wengi wamepata hasara”anasema Ramadhani
Akiuelezea ugonjwa huo anasema kuwa wakulima wanaofuga kuku wanapaswa kuwachanja wakiwa na wiki nne tangu wazaliwe ili kuweza kudhibiti maambukizi hayo.
Ramadhani anasema kuwa kuku au ndege akishapata ugonjwa huo macho huvimba na kupofuka hivyo kushindwa kula chakula na baadaye hufa kwa njaa.
Baada ya kuku kuugua mfagaji anatakiwa kumsafisha kuku macho kwa kutumia mafuta ya kula na kumpaka mafuta ya taa kila mara ili aweze kuona chakula vingenevyo anakufa na njaa.
“hakuna dawa nyingine ambayo anaweza kupewa lakini kama bado ni mdogo unaweza kumchanja dawa  aina ya Chicken pox Vaccine,..uhakika ni asilimia 80 kwamba hawataugua ugonjwa huo”anasema Rashid
Hata hivyo kauli hiyo imepingwa na mfugaji wa kuku mkazi wa kijiji cha Lunga, Seleman Rashid, ambaye amepoteza kuku 150 kutokana na ugonjwa huo.
Seleman anasema ugonjwa huo sio ndui bali ni mafua ya kuku ambayo humshambulia kuku kwa kutiririsha maji na machozi huku macho yakivimba nakuziba kabisa.
“unajua watalaamu wanatofautiana, mara ya kwanza hata mimi walinimbia ni ndui nikajiuliza mbona vifaranga vikitotolewa tu navichanja imetoka wapi ndui?”anahoji Rashid
Hata hivyo anasema baadaye aliwapiga picha na kwenda nayo kariakoo katika maduka makubwa yanayouza dawa za mifugo, walipoona tu hiyo picha wakamwambia hayo ni mafua ya ndege na alipopewa dawa ya ugonjwa huo wakaanza kupona.
Mtaalam mwingine aliyezungumzia ugonjwa huo ni John Chiwaligo ambaye amesema kuwa sio ugonjwa bali ni upungufu wa vitamin ndio unaosababisha kuku wanavimba macho.
Chiwaligo ambaye ni afisa ugani kata ya Lugoba amewashauri wafugaji wanaokumbana na ugonjwa huo wawape vitamin aina Multrivet.
“hiyo ni dalili kwamba kuku hao wanaukosefu wa vitamin mwilini,mfugaji  anapaswa kuwapa chanjo ya vitamin aina ya Tetrs Colvit au Multvet anawawekea kwenye maji wanakunywa”anasema Chiwaligo
Mtaalam huyo ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa chama cha wataalam wa mifugo nchini, anasema kuwa kuku akivimba macho anatakiwa kusafishwa kwa maji masafi na kuwekewa dawa aina ya macho aina ya Waund Powder.    
UGONJWA WA MAFUA YA KUKU (INFECTIOUS CORYZA
OR FOWL CORYZA

Ugonjwa wa kuku ni ugonjwa wa kuambukiza unaoshambulia zaidi mfumo wa juu wa upumuaji kwa kuku na baadhi ya ndege wa porini mfano njiwa.

 Ugonjwa huu  unasababishwa na bakteria wanaojulikana kitaalamu kama Avibacterium paragallinarum
(zamani aliitwa Hemophilus paragallinarum )
.
Ugonjwa wa mafua ya kuku unaweza kuwapata kuku wa umri wote lakini zaidi wale wa umri wa kati na wakubwa.

Aidha unajitokeza zaidi kwa kuku wanaotaga na wale wanaokaribia
kutaga mayai na mara chache hujitokeza kwa kuku wa nyama.
Uenezwaji Ugonjwa huu huenea kutoka kuku mmoja kwenda kwa kuku mwingine au kutoka banda/shamba moja kwenda jingine kwa njia ya kugusana kati ya kuku na kuku au watu wenye wadudu au kwa njia ya hewa kupitia chembe chembe ndogo za vumbi na pia kupitia maji ya kunywa.

Uenezwaji kwa njia ya vyombo vya chakula pia unawezekana.
Ugonjwa unaweza ukaanza na kuku wachache huku ukienea taratibu na kuishia na kuku wachache au uk
aenea kwa kasi na kushambulia kuku wengi.

 Ugonjwa unapatikana sehemu mbalimbali duniani na baadhi ya maeneo hujitokeza mara kwa mara. Kwa Tanzania ugonjwa huu hujitokeza hasa kuanzia mwezi wa tano hadi wa nane.

Dalili za Mafua ya kuku Kufuatia maambuzi ya ugonjwa huu, dalili huanza kujionyesha tangu siku ya 1 hadi ya 4. Dalili zake ni kama ifuatavyo:
-
Kwa ugonjwa wenye madhara madogo, dalili zinazoweza kuonekana ni kuzubaa, kuchuruzika mafua mepesi na mara chache kuvimba uso kwa kiasi kidogo.
-
Wakati ule ugonjwa mkali hujionyesha kwa kuvimba kwa kiasi kikubwa maeneo ya masikiona macho bpamoja na uwepo wa
maji kwenye nyama zinazozunguka maeneo ya macho inayopelekea kufumba kwa jicho moja au yote.

Kutoa makamasi mazito yaliyochanganyika na usaha puani
na mdomoni, vigubiko vya macho hushikana kwa ute mzito ambao huonekana pia ndani ya macho. Kwa kuku dume uvimbe unaweza kwenda hadi kwenye upanga/ndevu. Uvimbe huwa
mkubwa kati ya siku ya 10-14.
-
Dalili nyingine ni pamoja na kukohoa, kupumua kwa shida kunakosababisha watoe sauti ya mkwaruzo
(kukoroma),kuku kutoa machozi, kupungua kwa hamu ya kula
kunakowapelekea kushusha uzalishaji (ukuaji na utagaji wa mayai),kuharisha pia  kunaweza kutokea , kudhoofika na hatimaye kufa.Utagaji wa mayayi hushuka kwa
asilimia kuanzia 14 hadi 40. Kuku akipasuliwa
-
Utando mwepesi au mzito ndani ya pua, macho na masikio
wenye rangi ya njano,Uvimbe wenye maji maji maeneo ya usoni,
upanga/ndevu,na upande wa chini wa shingo
-
Uwepo wa wekundu na ukahawia au uchafu mweupe n
dani ya ngozi inayofunika
jicho
-
Uwepo wa rangi nyekundu kwenye kuta za koromeo la juu na ute mzito ndani yake,mara chache mapafu nayo huathirika.

Pia ufugaji kuku wakienyeji una faida kubwa zifuatazo; kuanzisha mradi hakuhitaji mtaji mkubwa sana, Kuku wa kienyeji hawahitaji eneo kubwa sana, kuku wa kienyeji wanastahimili mazingira magumu, Kuku wa kienyeji hawaugui mara kwa mara.

aidha kuku wa kienyeji wana soko kubwa sana, kuku wa kienyeji ana bei kubwa sokoni,Mayai ya kuku wa kienyeji ni mazuri sana, Mayai ya kuku wa kienyeji yana soko kubwa.
Faida ya kuku wa mayayi huanza kuonekana pale mfugaji anapokuwa na kuku 500 ambapo anakuwa na uhakika wa kukusanya trei 10 za mayai kwa siku.

Ukiweza kukusanya kiasi hicho cha mayai ya kienyeji unakuwa na uhakika wa kuuza kati ya shilingi 900 hadi 12000 kwa trei moja sawa na shilingi 90,000 kwa siku.

Hivyo kwa kipindi cha mwezi mmoja kama mfugaji atakuwa anauza kwa shilingi 90,000 ana  uhakika wa kuvuna kati ya shilingi milioni 2,700,000 hadi  milioni 3,60,000 kwa mwezi.
Pesa ambayo hata kama akitoa nusu yake kwa ajili ya kulipia gharama ya chakula na dawa bado mfagaji ana uhakika wa kubaki na kipato kikubwa zaidi ya wafanyakazi walioajiliwa au wafanyabiashara zingine   

CHANJO
Kuku wapewe chanjo ya kideri/mdondo kila baada ya miezi mitatu chanjo hii hupatikana nchini kote ukifika dukani ulizia chanjo ya newcastle, utapata maelekezo ya jinsi ya kuwawekea kuku kwenye maji ya kunywa, chanjo hii wapewe kuku wazima tu na wagonjwa watengwe mbali

MINYOO
Kuku hunyweshwa dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu, kuna dawa kama piperazine na nyinginezo ambazo huwekwa kwenye maji

CHAWA NA UTITIRI
Unaweza kutumia dawa za kuogeshea mifugo kama ecotix au dawa ya unga unga ya kunyunyuzia kama akheri powder, dawa ya akheri unaweza kuimwaga bandani na kisha kumnyunyuzia kuku mwilini ukiwa umemning’iniza kichwa chini miguu juu ili mayoya yaacha nafasi ya dawa kuingia

MAGONJWA YA MAPAFU
Kuna magonjwa mengi yanayoshambulia mfumo wa hewa, dawa ya tylosin inauwezo mkubwa wa kupambana na magonjwa karibu yote, wape dawa hii mara tu unapoanza kuona dalili za mafua
 Mayai ni chakula kilicho na madini muhimu na kisicho ghali katika soko lolote. (madini kama methionine na cystine), madini haya ni muhimu sana kwa afya ya watu hasa watoto wachanga.

Pia hutupatia protini,Kinyesi cha kuku ni mbolea safi pia ni kiwanda asilia cha kutotoa vifaranga.

Gharama za kuanzisha na kuendeleza miradi ni nyepesi, kitoweo chepesi na rahisi kwa wageni, kitoweo hakihitaji hifadhi hutumika mlo mmoja au miwili na kumalizika.

Jogoo hutumika kama saa inapowika,manyoya ya kuku hutumika kutengenezwa mapambo mbalimbali, mito na magodoro.

Kuku ndiye mnyama wa kipekee anayeweza kuishi mahali popote hapa ulimwenguni bila kuadhiriwa
na viwango vya hali ya hewa.

Ufugaji wa kuku ndio shughuli inayofanyika kwa wingi duniani kuliko ufugaji wa aina yeyote. Kuku hunawiri vyema katika nchi za hari kutokana na uwiano uliopatikana wakati wa mwanzo binadamu alipofuga Asian jungle fowl aina ya kuku-mwitu.

 Mayai pia yaweza kuhifadhiwa kwa urahisi na huchukua nafasi ndogo kuliko aina ya bidhaa zozote za mifugo. Mayai yaweza kuwekwa mahali kwa muda mrefu bila kuhitaji barafu.

 Kuku wanaolishwa nafaka baada ya kujitafutia chakula nje  huongeza idadi ya mayai (kutoka asilimia 20-25% hadi 40-50%).

TEKELEZA UTARATIBU WA KUZUIA MAGONJWA
Magonjwa ndio husababisha hasara katika mfumo wa ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi ya magonjwa hudumisha afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora kuliko kuponya.

 Kinga yaweza kutolewa mara kwa mara (kila baada ya miezi mitatu) dhidi ya magonjwa yafuatayo:

Ugonjwa wa Newcastle
Ugonjwa huu ndio huadhiri kuku na kusababisha hasara katika nchi za hari. Virusi vya ugonjwa huu huenea kwa kasi na rahisi kiasi cha kusababisha vifo kwa asilimia 100%. Dalili za kwanza ni shida ya kupumua na kung'amua hewa, sauti kama ya kikohozi na kutokwa mate.

 Kinyesi chaweza kuwa na rangi ya kijani kibichi. Hadi sasa hakuna dawa.
Waweza kuzuia ugonjwa huu kwa kutoa chanjo. Dawa za chanjo hupatikana kote ulimwenguni hata katika nchi za hari kwenye vipimo vya vitone mia moja. Madawa haya yaweza kuhifadhiwa kwa muda.

 Waweza kuweka kwa wiki moja mbali na jua au joto kali (Chanjo hii ni ya kipekee, kwani aina nyingine ya chanjo huwekwa kwa friji). Waweza kutoa chanjo kwa kutia vitone kwenye mdomo. Kuku wote (wakubwa kwa wadogo) wapaswa kupewa chanjo baada ya kila miezi mitatu.
Minyoo
Minyoo kama chango (roundworms) na tegu (tapeworms) huadhiri kuku wa kienyeji. Kuku hukosa hamu ya chakula, mayai hupungua na magonjwa mengine hushambulia. Ni bora basi kutoa minyoo.

Mchanganyiko wa madawa ya aina tatu ndio hutumiwa kuangamiza minyoo, madawa haya ni piperazine, phenothiazine na butynorate. Madawa haya hupatikana kama vidonge (tumia kidonge 1 kwa kuku mzima na 1/2 kwa vifaranga).

 Iwapo hautapata dawa hii, waweza kutumia Panacur au dawa nyingine ya kuangamiza minyoo. Wapatie kuku dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu.
Wadudu
Wadudu kama chawa au utitiri husumbua kuku katika ufugaji wa kienyeji. Chawa au utitiri husababisha harara ya ngozi, kuku walio adhiriwa hupata shida na kukosa usingizi.

 Hali hii hupunguza kiwango cha mayai na uzito wa kuku.
Tumia asilimia 5% ya unga wa malathion kwa kupulizia kuku (puliza kwa chupa uliyo toboa mashimo) pulizia kila kuku ili kuzuia chawa na utitiri (kilo moja ya unga huu yaweza kutibu kuku  150).

 Pulizia dawa hii baada ya kila miezi mitatu, waweza kupuliza kwa wakati mmoja wa kutoa chanjo na dawa zilizotajwa hapo juu. Puliza unga huu pia kwenye viota vya kuangulia mayai.

Waweza kutayarisha 5% ya malathion kwa kuchanganya 25% ya unga wa malathion (kiwango cha kilimo) na sehemu nne za jivu kutoka jikoni.
Magonjwa ya mapafu
Magonjwa ya mapafu huadhiri njia inayopitisha hewa na kuambatanisha mate na sauti kama ya kikohozi. Ugonjwa huu huenea polepole. Uambukizanaji pia hutokea kwa polepole na vifo sio kwa wingi.

 Hata hivyo, kutaga mayai na uzito hupungua. Shida hii yaweza kusambaa hata kutoka mahali vifaranga huanguliwa hadi pale walipouzwa. Tylosin19 ndio dawa inayoweza kutibu magonjwa ya mapafu.

 Kiasi cha 35mg ya tylosin hutosha kuku mmoja (kiwango hiki hufaa kuku na hata vifaranga) dawa hii husimamisha madhara kutokana na magonjwa ya mapafu. Tibu kuku kila baada ya miezi mitatu, waweza kutekeleza kwa wakati mmoja wa kutoa kinga na kuangamiza minyoo.

 Tylosin hupatikana kwa pakiti ndogo ya 4gm.
Waweza kutayarisha dawa hii kwa kutumia maji na 35gm ya tylosin (gramu nne kwa vikombe viwili

No comments: